Monday, November 4, 2013

IJUE ISTIQAAMA MUSLIM COMMUNITY OF TANZANIA

Istiqaama Muslim Community of Tanzania:
 Ni taasisi ya Kiibadhi ambayo ni kongwe inayoratibu miradi mbalimbali ya kusaidia uislamu pamoja na kutoa elimu ya dini ya kiislamu, usimamizi wa zaka, kuandaa mashindano ya Qur aan na kueneza uislamu,kusimamia na kuendesha madrasa, shule na vituo vya kulelea mayatima, kupokea michango,sadaka na kuwatafutia vijana wa kiislamu nafasi za masomo ya elimu ya juu katika vyuo mbalimbali vya serikali na binafsi vilivyopo nchini na nje ya nje.
Istiqaama imeweza kujenga misikiti na madrasa na shule karibu nchi nzima, katika mikoa ya
Dar es salaam, Tanga, Shinyanga na Tabora, Dodoma, Mwanza, Sumbawanga na Kigoma na Bukoba na Unguja na Pemba na Mbeya. Pia imeweza kujenga hospitali Unguja na hospitali maarufu na bora ya wanawake jijini Dar es salaam iliyopo katika eneo la Magomeni Kagera.





Blog hii itakuwa inaonyesha harakati mbalimbali za Istiqaama pamoja na harakati za dini ya Kiislamu nchini Tanzania
LENGO SIO KUIPAMBA NA KUITANGAZA ISTIQAAMA BALI NI KUITANGAZA NA KUIPIGANIA DINI YA KIISLAMU KWA KUTUMIA NJIA NZURI ITAKAYODUMISHA AMANI YA NCHI YETU YA TANZANIA NA PIA KUIMARISHA MAENDELEO YA UISLAMU KUPITIA NYANJA MBALIMBALI ZA MAENDELEO SANJARI NA KUTOA HUDUMA MBALIMBALI KATIKA JAMII YETU YA TANZANIA KWA WAISLAMU NA WASIOKUWA WAISLAMU KATIKA SUALA ZIMA LA ELIMU NA ELIMU KWA WALIOATHIRIKA NA MAYATIMA PAMOJA MATIBABU.

Masjid Istiqaama uliopo Tandika - Dar es salaam

Masjid Al -  Khalily ulipo Magomeni Kagera jijini Dar es salaam

Maktaba ya vitabu vya dini ya Kiislam iliyopo katika Masjid Istiqaama Ilala.

Mmoja wa Waumini wa dini ya kiislamu akijisomea katika Maktaba ya Istiqaama Ilala.

Moja katika madrasa nzuri na ya kisasa ya dini ya kiislamu iliyopo katika Masjid Istiqaama Ilala.

Mwenyekiti wa Kamati ya vijana Istiqaama Dar es salaam, Sheikh Saleh Omar akiwakagua wanafunzi wa madrasa bora ya kuhifadhi Qur aan iliyopo katika Masjid Istiqaama Ilala.

Mhadhiri wa kutoka Misri akitoa mhadhara katika moja ya mihadhara iliyoandaliwa na Kamati ya vijana wa Istiqaama Tanzania, kulia kwake ni mkalimani ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya vijana ya Istiqaama Mwanachuoni Sheikh Saleh Omar
 
KHERI NA BARAKA ZA 1435 HIJRIYYAH KUTOKA KWA ALLAH ZIWE JUU YENU:
Jumuiya ya ISTIQAAMA ya tanzania, tawi la Dar-es-Salaam, ina furaha kubwa kuwaalika nyote (wanaume na wanawake) katika HAFLA kubwa, fupi na ya aina yake, ya kuupokea mwaka mpya wa kiislamu 1435 Hijriyaah, siku ya Jumapili tarehe 10 Novemba, 2013 katika ukumbi wa Karimjee, kuanzia saa 3 kamili asubuhi mpaka saa 6 kamili mchana.. MGENI RASMI Inshaa ALLAAH atakuwa Mheshimiwa Dk. Mohammed Gharib Bilal
(Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania) nyote mnakaribishwa








No comments:

Post a Comment