Thursday, November 14, 2013

Makamu wa Rais wa Tanzania ajumuika na waislamu katika hafla ya kuukaribisha mwaka mpya wa kiislamu 1435 Hijriyyah.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwasili kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam,  kwa ajili ya kuhudhuria hafla ya kuupokea mwaka mpya wa Kiislamu 1435 Hijriyya huku akilakiwa na waumini, kulia kwake ni wana Kamati ya vijana Sulaiman Sharjiy na Muthanna H. Al Shaibaniy.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia katika hafla ya sherehe za kuukaribisha mwaka mpya wa Kiislamu 1435 Hijriyya
 

Makamu wa Rais akisalimiana na Sheikh Ali Suleiman Al Kharousy, katikati anayeshuhudia ni Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Sheikh Alhaad Musa Salum

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akisalimiana kwa furaha na Mwenyekiti wa Kamati ya vijana Istiqaama Sheikh Saleh Omar Attiwaaniy huku akishuhudiwa na Sheikh Hafidh Attiwaaniy na Sheikh Ali Suleiman Al Kharousy

Sheikh Saleh Omar akijadiliana jambo na Balozi wa Egypt nchini Mheshimiwa Hossam Moharram

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dr. Mohammed Gharib Bilal akipeana mkono na Sheikh Saleh Omar Attiwaaniy na katikati anayeshuhudia ni mtunzi mahiri wa vitabu vya dini ya Kiislamu katika zama hizi Sheikh Khalfan Sulaiman Attiwaaniy Allah S.W amjaalie umri mrefu na wenye kheri na baraka

 Sheikh Saleh Omar akiwa na Mheshimiwa Shamim Khan ambae mchango wake ulikuwa mkubwa katika serikali ya nchi yetu ya Tanzania na pia katika harakati mbalimbali za uislamu nchini.

Sheikh Saleh Omar akipena mkono na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Mheshimiwa Dr. Gharib Bilal

Wageni waalikwa wakiitikia dua iliyosomwa na Sheikh Ahmed Mohammed Al Badry

 Kumbukumbu ya Picha ya Hafla ya Mwaka 1435 Hijriyya, picha iliyopigwa nje ya Ukumbi wa Karimjee
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Sheikh Alhaad Musa Salum akimpa zawadi Makamu wa Rais wa Tanzania kwa kutambua mchango wake katika kufanikisha hafla ya kupokea mwaka mpya wa kiislamu 1435 Hijriyyah

Makamu wa Rais wa Tanzania akijadili jambo na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam

Sehemu ya waumini wa dini ya Kiislamu,waliohudhuria hafla ya kuupokea mwaka mpya wa Kiislamu 1435 Hijriyya, wakiitikia dua iliyosomwa na Sheikh Ahmed Mohammed Al Badry, katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam

 
 Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhad Mussa Salum, akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Makamu wa Rais, Dkt. Bilal, kuhutubia hadhira iliyofika katika hafla hiyo.

Monday, November 4, 2013

ISTIQAAMA MWANZA WAFANYA MAJLIS YA KUUKARIBISHA MWAKA MPYA WA KIISLAMU

Istiqaama Mwanza wamefanikiwa kufanya Majlis ya kuukaribisha mwaka mpya wa Kiislamu pamoja na kuadhimisha Hijra ya Mtume wetu Muhammad (S.A.W), kwa mujibu wa Sheikh Nuuh majlis hiyo ilifanyika leo Tarehe 4 Novemba 2013 katika Msikiti wa Ibaadh Mwanza na kuhudhuriwa na vijana na wazee mbalimbali kutoka madhehebu mbalimbali katika Jiji la Mwanza

PICHA ZA MATUKIO YA TAMASHA LA EID EL FITRI YA MWAKA 1431

Hakika ilikuwa furaha kwa kila mmoja aliyebahatika kuhudhuria sherehe za Tamasha la Eid el fitr mwaka 1431 Hijria, lakini siku hazirudi nyuma bali zinaenda mbele, bali kumbukumbu ya matukio ya picha ndio yanayoturudisha nyuma kufurahia yale mazuri ambayo yaliyopita, Nafsi zetu kujiuliza hizi sherehe zilikuwa za mwaka 1431 wakati huo kamati ya vijana ya Istiqaama ilikuwa changa mno, je sherehe za Tamasha la Eid 1435 inshaallah zitakuwa katika ubora upi?, miaka 4 imepita tokea Tamasha hili lilipofanyika, kwani Kamati ya vijana Istiqaama imezidi kuwa na uzoefu na hivi sasa ina vijana imara katika kusimamia dini ya Allah s.w, kila mmoja wetu akijaaliwa uhai na afya inshaallah ajitahidi kuhudhuria katika sherehe za Tamasha la Eid el Fitri 1435 mwaka na amtaarifu kila mmoja ambaye hajawahi kuhudhuria sherehe hizo za Tamasha la Eid zinazofanyika katika viwanja vya Dar es salaam ZOO kila mwaka.
Wageni walioalikwa Masheikh kutoka Misri ambao pia ni waalimu wa chuo cha Markaz na Sheikh Al haad Musa ambaye ni Sheikh wa Mkoa wa Dar es salaam


















Hakika zawadi zilikuwa za aina yake ambazo zilizidisha furaha ya sherehe za eid kwa wale walioshinda, huenda inshaallah sherehe zijazo za mwaka 1435 kutakuwa na zawadi ya Flat screen na ikiwepo naona shindano litakuwa la kusisimua mno. 

HAFLA YA KUUPOKEA MWAKA MPYA WA KIISLAMU 1435 HIJRIYYAH

KHERI NA BARAKA ZA 1435 HIJRIYYAH KUTOKA KWA ALLAH  ZIWE JUU YENU:

IJUE ISTIQAAMA MUSLIM COMMUNITY OF TANZANIA

Istiqaama Muslim Community of Tanzania:
 Ni taasisi ya Kiibadhi ambayo ni kongwe inayoratibu miradi mbalimbali ya kusaidia uislamu pamoja na kutoa elimu ya dini ya kiislamu, usimamizi wa zaka, kuandaa mashindano ya Qur aan na kueneza uislamu,kusimamia na kuendesha madrasa, shule na vituo vya kulelea mayatima, kupokea michango,sadaka na kuwatafutia vijana wa kiislamu nafasi za masomo ya elimu ya juu katika vyuo mbalimbali vya serikali na binafsi vilivyopo nchini na nje ya nje.
Istiqaama imeweza kujenga misikiti na madrasa na shule karibu nchi nzima, katika mikoa ya
Dar es salaam, Tanga, Shinyanga na Tabora, Dodoma, Mwanza, Sumbawanga na Kigoma na Bukoba na Unguja na Pemba na Mbeya. Pia imeweza kujenga hospitali Unguja na hospitali maarufu na bora ya wanawake jijini Dar es salaam iliyopo katika eneo la Magomeni Kagera.





Blog hii itakuwa inaonyesha harakati mbalimbali za Istiqaama pamoja na harakati za dini ya Kiislamu nchini Tanzania
LENGO SIO KUIPAMBA NA KUITANGAZA ISTIQAAMA BALI NI KUITANGAZA NA KUIPIGANIA DINI YA KIISLAMU KWA KUTUMIA NJIA NZURI ITAKAYODUMISHA AMANI YA NCHI YETU YA TANZANIA NA PIA KUIMARISHA MAENDELEO YA UISLAMU KUPITIA NYANJA MBALIMBALI ZA MAENDELEO SANJARI NA KUTOA HUDUMA MBALIMBALI KATIKA JAMII YETU YA TANZANIA KWA WAISLAMU NA WASIOKUWA WAISLAMU KATIKA SUALA ZIMA LA ELIMU NA ELIMU KWA WALIOATHIRIKA NA MAYATIMA PAMOJA MATIBABU.

Masjid Istiqaama uliopo Tandika - Dar es salaam

Masjid Al -  Khalily ulipo Magomeni Kagera jijini Dar es salaam

Maktaba ya vitabu vya dini ya Kiislam iliyopo katika Masjid Istiqaama Ilala.

Mmoja wa Waumini wa dini ya kiislamu akijisomea katika Maktaba ya Istiqaama Ilala.

Moja katika madrasa nzuri na ya kisasa ya dini ya kiislamu iliyopo katika Masjid Istiqaama Ilala.